'Inawezekana kuyakamilisha Malengo ya Milenia 2015' asisitiza KM
Kwenye mahojiano na Redio ya UM Ijumanne, KM Ban Ki-moon alisisitiza kwamba anaamini walimwengu wapo kwenye mkondo sawa hivi sasa ambao utawawezesha kuyakamilisha Malengo ya Maendeleo ya Milenia kwa wakati.