Skip to main content

Tume juu ya tukio la Beit Hanoun yawakilisha ripoti katika HRC

Tume juu ya tukio la Beit Hanoun yawakilisha ripoti katika HRC

Hii leo mjini Geneva kwenye ukumbi wa Baraza la Haki za Binadamu (HRC), Askofu Mkuu wa Afrika Kusini Desmond Tutu aliwakilisha ripoti ya mwisho juu ya matokeo ya uchunguzi waliofanya tume aliyoiongoza, ya hadhi ya juu, kuhusu shambulio la mwezi Novemba 2006 kwenye eneo la Wafalastina liliokaliwa kimabavu na Israel la Beit Hanoun, liliopo katika Tarafa ya Ghaza, ambapo raia 19 waliuawa na mizinga ya wanajeshi wa Israel.

Kwa taarifa zaidi kuhusu fafanuzi za Askofu Mkuu Tutu juu ya athari za tukio hilo kwa umma wa KiFalastina katika Tarafa ya Ghaza, sikiliza idhaa ya mtandao.