Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF-WHO yawasiliana na Uchina kudhibiti maradhi yaliotokana na maziwa ya unga

UNICEF-WHO yawasiliana na Uchina kudhibiti maradhi yaliotokana na maziwa ya unga

Mashirika ya UM juu ya maendeleo ya watoto, UNICEF, na afya ya kimataifa, WHO, yameripoti kwamba hivi sasa yanawasiliana, kwa ukaribu zaidi, na Wizara ya Afya ya Uchina ili kufuatilia tatizo la afya liliozuka nchini karibuni maziwa ya unga ambayo yameshadhuru maelfu ya watoto wachanga.

Mashirika ya WHO na UNICEF yamependekeza mama wazazi wanyonyeshe watoto wachanga badala ya kutumia maziwa ya unga, kwa sababu imeshathibitishwa kitaaluma ya kuwa maziwa ya mama ndio yenye virutubisho vya chakula vinavyomsaidia mtoto awe na afya bora.