Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale (Taarifa za Kusoma)

Hapa na pale (Taarifa za Kusoma)

Mohamed ElBaradei, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) Ijumatatu aliwaambia wajumbe wa Bodi la Magavana wa taasisi waliokutana Vienna, kwamba wakaguzi wake wameweza kuthibitisha Iran haijabadilisha matumizi ya nyuklia kinyume na dhamira ilioripotiwa nao. Kadhalika ElBaradei alisema IAEA haikufanikiwa kuthibitisha madai ya baadhi ya mataifa kwamba mradi wa nishati ya nyuklia wa Iran, unafungamana na shughuli za kijeshi. Aliyataka yale Mataifa Wanachama yenye kudai kuwa na ushahidi mradi wa Iran wa nyuklia hutumiwa kwenye shughuhuli za siri za kijeshi yaipatie IAEA ushahidi huo ili uthibitishwe na wataalamu wake kama ni ushahidi wa kweli au la.

Shirika la M juu ya Mfuko wa Maendel;eo kwa Watoto (UNICEF) umetangaza ombi maalumu lenye kusihi kundi la waasi la LRA kuwaachia huru haraka, na bila shuruti, watoto 90 waliowateka nyara wiki iliopita. UNICEFinakhofia watoto hao huenda wakalazimishwa kupigana na kuhatarisha maisha yao. Utekaji nyara wa watoto hawa ulitukia baada ya vijiji kuhujumiwa na waasi kwenye Jimbo la Orientale. Vile vile UNICEF chifu mmoja wa kijiji alitekwa nyara pamoja na mamishionari wa Kitaliana wawili, wakati raia 3 waliuawa, vituo vya afya viliibiwa na mji wa Kiliwa uliteketezwa kwa moto. Watu walionusurika na tukio hilo walikimbilia vijiji vya jirani na UNICEF inajitahidi kukidhi mahitaji ya dharura yaliochochewa na mzzo huo. Wakati huo huo Shirika la Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limeripoti mnamo mwisho wa wiki iliopita hadi asubuhi leo mapigano ya kutumia silaha nzito yaliendelea katika jimbo la kaskazini-mashariki kati ya vikosi vya Serikali na waasi wanaoongozwa na Jenerali Mtoro Laurent Nkunda.