Raisi wa Tanzania azingatia umuhimu wa Malengo ya Milenia kukuza maendeleo Afrika

25 Septemba 2008

Raisi Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, kwenye taarifa alioitoa mbele ya wajumbe waliohudhuria kikao cha Baraza Kuu (BK) juu ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), alitilia mkazo “umuhimu mkubwa mno” wa mkusanyiko wao. Alikumbusha ya kwamba mnamo tarehe 22 Septemba KM aliitisha mkutano wa ngazi ya juu kuzingatia mahitaji ya kukuza huduma za maendeleo katika bara la Afrika.

"Mwito ulitambua kwamba ufukara na hali duni ya kijamii barani Afrika ndio vizingiti vikubwa vinavyokwamisha maendeleo, na kunahitajika maendeleo maridhawa na uchumi wa kusarifiwa ili kuushinda ufukara. Mwito ulitilia mkazo utekelezaji wa zile ahadi zilizopita, na za sasa, za kushirikiana kipamoja katika kukidhi mahitaji ya kukuza huduma za maendeleo ya siku za usoni katika Afrika, kwa kulingana na maadili asilia ya Umoja wa Mataifa. Mwito ulisisitiza uhalali wa ule mfumo wa Ushirikiano Mpya kwa Maendeleo ya Afrika, yaani mfumo wa NEPAD ambao hujumlisha taratibu zinazotakikana kudumisha maendeleo ya uchumi na kijamii katika bara la Afrika. Mwito huu muhimu unahimiza utekelezaji kamili, na kwa wakati, wa mapatano yote ya kimataifa kuhusu malengo ya maendeleo, ikijumlisha Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs)."

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter