WHO inahimiza mama wazazi wanyonyeshe watoto wachanga kuwanusuru na maradhi ya utotoni

1 Agosti 2008

Kuanzia tarehe mosi hadi 7 Agosti nchi 120 ziada zitashiriki kwenye kampeni maalumu ya kuhamasisha mama wazazi wa kimataifa kunyonyesha watoto, hasa katika miezi sita ya kwanza baada ya kuzaliwa, kipindi ambacho imethibitika maziwa ya mama humsaidia kumpatia mtoto kinga na afya bora dhidi ya maambukizo maututi ya maradhi ya utotoni kama ugonjwa wa kupumua na kuharisha. Kampeni hii imeandaliwa na Shirika la Umoja wa Dunia Kuendeleza Unyonyeshaji (WABA). Miongoni mwa mashirika yanayojihusisha na huduma hii ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) na pia Shirika la Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) wakijumuika na wadau wengine wa kimataifa.

Mashirika ya UM ya UNICEF na WHO yanasaidiana kipamoja kuhudumia miradi mbalimbali yenye kuhimiza mama wazazi kunyonyesha watoto wao, ikijumuisha miradi ya mafunzo maalumu juu ya namna ya kuwalisha watoto wachanga na watoto wadogo, na pia mafunzo ya visaidizi vinavyotakikana kuendesha shughuli za wahudumia afya na washauri wa afya, hali kadhalika.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter