KM na Mkuu wa UNAIDS wafungua rasmi Kijiji cha Dunia, Mexico City, kuzingatia masuala ya UKIMWI
KM BAN Ki-moon pamoja na Dktr Peter Piot, Mkurugenzi wa Jumuiya ya Mashirika ya UM Dhidi ya UKIMWI (UNAIDS) wamefungua rasmi kwenye Mkutano wa Mexico City juu ya UKIMWI kijiji kinachojulikana kama Kijiji cha Dunia, sehemu ya kilomita 8,000 za mraba, ambayo itatumiwa na maelfu ya wajumbe wanaohudhuria kikao hicho kujadiliana na kubadilishana mawazo na uzoefu, pamoja na kujenga muungano wa mitandao, ili kurahisisha majukumu ya kupiga vita kipamoja UKIMWI kote duniani. ~~