Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kanada kutuma manowari Usomali kulinda meli za chakula za WFP

Kanada kutuma manowari Usomali kulinda meli za chakula za WFP

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limetangaza kukaribisha uamuzi wa serikali ya Kanada wa kupeleka manowari kwenye mwambao wa Usomali, itakayotumiwa kusaidia kulinda zile meli zinazochukua shehena ya chakula inayopelekwa umma wa Usomali kunusuru maisha. Meli hizo huwa zinakodiwa na WFP na mara nyingi hutekwa nyara na maharamia wanaovizia kwenye mwambao wa Afrika Mashariki katika Bahari ya Hindi.