Jumuiya za NGOs zatunukiwa riboni nyekundu kwa juhudi zao dhidi ya UKIMWI
Hii leo kwenye Mkutano Mkuu wa Kimataifa juu ya UKIMWI unaofanyika Mexico City, Mexico mashirika 25 yasio ya kiserekali (NGOs) yametunikiwa zawadi maalumu inayojulikana kama Tunzo ya Utepe Mwekundu/Riboni Nyekundu kwa mchango wao muhimu kwenye zile juhudi za kutibu UKIMWI kwenye jamii zao, na katika kuimarisha haki za waathiriwa wa magonjwa hayo. Vile vile walitunukiwa tunzo hizo kwa kuamsha hisia za jamii zao juu ya ulazima wa dharura unaotakikana kujikinga na maambukizo ya VVU na kudhibiti bora janga hili maututi. ~