Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UPU kusaidia Utawala wa Wafalastina kuhudumia operesheni za posta

UPU kusaidia Utawala wa Wafalastina kuhudumia operesheni za posta

Shirika la Muungano wa Posta Ulimwenguni (UPU) limetangaza kwamba wasimamizi wa mamlaka ya posta katika Israel na Falastina wanashauriana sasa hivi kuhusu taratibu za kurahisisha operesheni za posta za Utawala wa Falastina kati ya eneo liliokaliwa kimabavu na nchi za nje.