Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wenyeji wa asili wanahatarishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, FAO inahadharisha

Wenyeji wa asili wanahatarishwa na mabadiliko ya hali ya hewa, FAO inahadharisha

Kwenye mkesha wa kuadhimisha \'Siku Kuu ya Kimataifa kwa Wenyeji wa Asili\' Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeonya hali haribifu na ngumu ya mazingira inayoongezeka kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, pamoja na upungufu wa haki za kumiliki ardhi na rasilmali nyengine za kimsingi, ni masuala yanayoashiria kuhatarisha maisha na pia njia za kujipatia rizki kwa fungu kubwa la makundi ya wenyeji wa asili duniani, makundi ambayo utulivu bora wa maisha yao ndio yenye ufunguo wa kudumisha maisha ya kuridhisha kwetu sote kote ulimwenguni.