Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UNAMID juu ya shambulio la raia na shughuli za usalama katika Darfur

Ripoti ya UNAMID juu ya shambulio la raia na shughuli za usalama katika Darfur

Vikosi vya Mseto vya UM/UA kwa Darfur, vinavyojulikana kwa umaarufu Vikosi vya UNAMID viliwasilisha ripoti iliotibitisha tukio ambalo lilisababisha vifo na majeruhi kadha ya raia. Kwa mujibu wa ripoti, magari saba ya raia yaliokuwa yamepakia Wasudani, yaliokuwa yakisafiri kutoka Nyala kuelekea ElFasher, yalishambuliwa kwa kuvizia na watu wasiojulikana waliokuwa wamepanda ngamia, ambao wanadaiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la Janjaweed.

UNAMID pia imeripoti askari 170 wa Vikosi vya Gambia waliwasili El Fasher Ijumatano kuanzisha operesheni za doria ili kulinda usalama wa kambi za UNAMID ziliopo Darfur.

Wakati huo huo wanajeshi wahandisi wa kutoka Misri wanatarajiwa kuwasili El Fasher mnamo tarehe 12 Agosti kujiunga na wenziwao walioenezwa Darfur katika siku za nyuma, na kusaidia ujenzi wa miundombinu ya kuimarisha operesheni za UNAMID kieneo.