Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Shirika la Mchanganyiko juu ya Ulinzi Amani la UA/UM (UNAMID) limeripoti moja ya helikopta zake ilipigwa risasi adhuhuri katika Darfur Magharibi, nusu saa baada ya kupaa kutokea mji wa El Geneina. Rubani wa helikopta alilazimika kutoendelea na safari na kuamua kurejea El Geneina, kilomita 90 kutoka eneo la tukio hilo. Hakuna mtu aliyejeruhiwa na helikopta inafanyiwa uchunguzi. Haijulikani sasa hivi ni nani aliyehusika na kiutendo hicho.

Shirika la Ulinzi wa Amani la UM katika Cote d'Ivoire (UNOCI)limepeleka bechi ya kwanza ya vifaa 1,500 vya uchaguzi kukabidhi Serikali kutokea ghalaza UM ziliopo Brindisi, Utaliana. Vifaa hivi vinatarajiwa kusaidia kuharakisha uchunguzi wa vitambulisho vya wapiga kura.