Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

NKM asisitiza dhamana ya mawakili kutunza haki za raia

NKM asisitiza dhamana ya mawakili kutunza haki za raia

Naibu KM wa UM, Asha-Rose Migiro alipohutubia Chama cha Mawakili wa Amerika (ABA) mjini New York Ijumapili alitoa mwito maalumu ulihimiza mawakili kukuza mchango wao unaohitajika kuhakikisha nchi wanachama zinatekeleza ahadi za kukinga raia dhidi ya mauaji ya halaiki, jinai ya vita, utakaso wa kimila na makosa ya jinai dhidi ya utu.