Ripoti fupi kuhusu mzozo wa Ossetia Kusini

12 Agosti 2008

Hali ya eneo la machafuko na vurugu katika jimbo liliojitenga la Georgia, katika Ossetia Kusini, inaendelea kuwa ya vurugu na utumiaji nguvu, na UM haukufanikiwa kuhudumia kihali umma raia waathiriwa wa mzozo huo kama inavyopaswa.~~ Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti kunahitajika kufunguliwa ushoroba mpya wa usalama utakaotumiwa na magari ya mashirika ya kimataifa kupeleka misaada ya kiutu kwenye eneo la mapigano.

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) imetangaza kupokea dola miloni 7.4 kukidhi mahitaji ya dharura ya matibabu kwa watu 50,000 waliodhuriwa na mapigano katika Ossetia Kusini. Hivi sasa ICRC inajitayarisha kupeleka tani 16 za vifaa vya kuhudumia matibabu kwenye eneo la vurugu itakapopokea kibali cha kuelekea huko. ICRC pia imeripoti marubani wawili wa KiRusi waliopewa ruhusa ya kuwatumikia kikamilifu kusafirishia vifaa vya misaada ya kihali, marubani hao wapo kizuizini nchini Georgia. Kwa mujibu wa ICRC hali za marubani wa Kirusi ni nzuri na aila zao pampja na Ubalozi wa Urusi uliopo Tbilisi wamesharifiwa na ICRC kuhusu hali yao. ICRC vile vile imetoa ombi la kuruhusiwa kuwazuru watu wote waliotiwa kizuizini, kukamatwa au kutekwa kwenye mapigano.

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetangaza litaendelea kushauriana na mashirika mengine ya UM yaliopo kwenye eneo la mgogoro juu ya nidhamu za kuchukuliwa kuwasaidia wale watoto walio peke yao na wenye kuhitajia hifadhi ya kimataifa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter