Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Aina mpya ya Homa ya Mafua ya Ndege imegunduliwa Nigeria

Aina mpya ya Homa ya Mafua ya Ndege imegunduliwa Nigeria

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limetangaza kuzuka aina mpya ya virusi vinavyosababisha Homa ya Mafua ya Ndege katika Nigeria, uzao ambao haujawahi kushuhudiwa hapo kabla katika mataifa ya Afrika yaliopo Kusini ya Sahara. Virusi hivi vimegunduliwa katika majimbo ya Katsina na Kano, na baada ya kufanyika uchunguzi kwenye maabara za serikali, kwa ushirikianao na FAO na watalamu wa afya za wanyama imethibitishwa kuwa ni virusi hatari vyenye kusababisha ugonjwa wa Homa ya Mafua ya Ndege.