Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vikosi vya wahandisi wa Misri vimewasili Darfur kuhudumia miundombinu

Vikosi vya wahandisi wa Misri vimewasili Darfur kuhudumia miundombinu

Shirika la Mchanganyiko la UM/UA kwa Darfur (UNAMID) limeripoti Ijumanne wamewasili Darfur wanajeshi wahandisi 129 wa Misri, vikosi ambavyo vitakamilisha Kampuni ya Askari Wahandisi 335 wa Misri waliopangwa kuhudumia miundombinu ya ulinzi wa amani katika eneo la uahasama.Wanajeshi hawa watafuatiwa mwisho wa wiki na askari wa UNAMID kutokea Ethiopia.