Shambulio la bomu Lebanon lalaaniwa na BU na KM
Baraza la Usalama pamoja na KM wamelaani kwa lugha nzito shambulio la bomu liliotukia katika mji wa Tripoli, Lebanon Ijumatanao asubuhi ambapo iliripotiwa watu 10 waliuaawa na askari kadha kujeruhiwa. Risala ya KM ilisema anatumai tukio hili halitotumiwa na maadui wa amani kuzorotisha maendeleo ya kisiasa yaliojiri Lebanon katika kipindi cha karibuni, ambapo hali ya maisha ya kawaida ilikuwa inanyemelea kurejea nchini. ~