Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mipango 1,000 ya maendeleo kuanzishwa na UM Cote d'Ivoire

Mipango 1,000 ya maendeleo kuanzishwa na UM Cote d'Ivoire

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika Cote d\'Ivoire (UNOCI) limeanzisha mradi mpya wa dola milioni 5 kuharakisha juhudi za kuwaunganisha kwenye huduma za jamii na maendeleo wale wapiganaji wa zamani walioshiriki kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini, pamoja na vijana waliokosa ajira.