Mkuu wa UNHCR kuanza ziara Georgia na Urusi kusailia mahitaji ya kiutu kieneo

19 Agosti 2008

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa Shirika la UM Juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) amewasli Tbilisi Ijumanne kuanza ziara ya siku nne katika Georgia na, baadaye kueleka Shirikisho la Urusi kutathminia mahitaji ya wahamiaji walioathirika na vuruugu lilizouka katika wiki za karibuni kieneo.~~

Guterres baada ya kuwasili Georgia alitoa mwito maalumu kwa jumuiya ya kimataifa unaowahimiza kukithirisha michango maridhawa ya kuhudumia kidharura umma ulioathiriwa na mapigano yaliofumka majuzi nchini humo.

Alasiri Baraza la Usalama lilikutana kwa mashauriano kuzingatia hali katika Georgia.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter