Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM inawakumbuka watumishi wajasiri na mashujaa walioshambuliwa Baghdad miaka mitano iliopita

UM inawakumbuka watumishi wajasiri na mashujaa walioshambuliwa Baghdad miaka mitano iliopita

Ijumanne asubuhi kulifanyika taadhima maalumu Makao Makuu za kuhishimu kumbukumbu ya shambulio la ofisi za UM katika Hoteli ya Canal mjini Baghdad, ambapo mnamo tarehe 19 Agosti 2003, miaka mitano nyuma, lori liliobebeshwa mabomu liliegezwa kwenye majengo ya UM na kuripuliwa.

Taadhima za kumbukumbu ya shambulio la ofisi za UM Baghdad ziliandaliwa na Kamati ya kudumu juu ya Usalama na Uhuru wa Wafanyakazi wa Kimataifa kwa makusudio ya kuamsha hisia za kimataifa kuhusu hatari watumishi wa UM hukabiliwa nazo kila kukicha, katika sehemu mbalimbali za dunia wakati wanapojitahidi kukamilisha maadili ya UM ya kukuza maendeleo, kuimarisha usalama na amani na kuhishimu haki za binadamu kwa wote, kote duniani.

“Wimbo Usio Mipaka” ulitumbuizwa mkusanyiko wa taadhima hizo na kundi la wanamuziki wanne wanaojiita 'Daedalus Quartet'.