Hapa na pale

20 Agosti 2008

Baraza la Usalama Ijumatano lilikutana tena kusailia tatizo sugu la Mashariki ya Kati, ikijumuisha suala la haki za WaFalastina.~~

Mshauri Maalumu wa KM kwa Masuala ya Myanmar, Ibrahim Gambari - ambaye amekamilisha siku ya tatu ya ziara yake nchini huko - alikutana Ijumatano na mawaziri wa Mipango na Afya na kujadiliana nao hali ya kiuchumi na jamii. Kadhalika Gambari alifanya mikutano 10 mbalimbali na wawakilishi wa vyama vya kisiasa na jumuiya za kiraia, ikijumuisha wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Umoja wa Taifa kwa Demokrasia, na kukutana na wawakilishi wa vyama vya wanafunzi pamoja na watu waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa 1990. Walisailia juu ya umuhimu wa kuwepo mazungumzo ya upatanishi ya kitaifa, mfumo unaoaminika wa kisiasa na taratibu madhubuti za kukabiliana, kwa mafanikio, na matatizo ya kiuchumi na jamii.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter