Hifadhi ya makasa wa baharini imetia gia kuu, yasema UNEP

20 Agosti 2008

Ripoti iliowasilishwa leo kwenye mkutano unaofanyika Bali, Indonesia kuhusu hifadhi ya makasa wa baharini waliopo kwenye maeneo ya Bahari ya Hindi na Asia ya Kusini-Mashariki, ilibainisha kupatikana maendeleo ya kutia moyo miongoni mwa yale mataifa 27 yaliotia sahihi maafikiano ya kuwalinda wanyama hawa dhidi ya uharibifu wa mastakimu yao.

Miongoni mwa mataifa yanayohudhuria mkutano wa Bali ambayo yalijizatiti kusimamia hifadhi ya makasa wa bahari kwa muda mrefu ni pamoja na Australia, Oman, Ushelisheli na pia Afrika Kusini. Mkutano utaendelea Ijumamosi tarehe 23 Agosti 2008.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter