Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msanii S. Heitzeg aifadhilia UM hidaya ya utunzi wa 'Wimbo usio Mipaka'

Msanii S. Heitzeg aifadhilia UM hidaya ya utunzi wa 'Wimbo usio Mipaka'

Mapema Ijumatano asubuhi ya tarehe 19 Agosti 2008 walikusanyika Makao Makuu ya UM aila ya UM - ikijumuisha KM BAN Ki-moon - kwenye taadhima maalumu za kumbukumbu ya mwaka wa tano tangu ofisi za UM ziliporipuliwa kwa bomu liliopakiwa lori iliogeshwa karibu na majengo ya Hoteli ya Kanali, yalipokuwa ofisi za UM mjini Baghdad. Shambulio lilitukia tareheb 19 Agosti 2003.

Mwandishi habari wa Redio ya UM, Bissera Kostova alibahatika kufanya mahojiano na msanii Steve Heitzeg na miongoni mwa masuala aliyomwuliza ni kutkakujua vipi yeye binafsi alisikia na kuathirika na shambulio la Ofisi za UM Baghdad miaka mitano nyuma?:

"Ni dhahiri nilisikia kutoka TV na kwenye magazeti. Nilifadhaika sana. Siku zote nilikuwa na imani kubwa kuhusu maadili ya kazi za UM, na nilijuwa ajali hiyo ilikuwa msiba mkubwa kwa UM wenyewe. Ilivyokuwa mimi ni mfuasi wa itikiadi ya kupinga vita, kwa miaka kadha, kitendo hiki cha Baghdad kisio maana, bila shaka kilikuwa ni hasara kuu kwa watu waliopoteza maisha. Kwa hivyo nilihisi - kwa kupitia muziki ninayotunga - siku zote nikiamini ya kwamba muziki na usanii ni mambo pacha ambayo tungeweza kuyatumia kuimarisha amani ulimwenguni. Muziki ni lugha ya watu wote, huunganisha ubinadamu wetu sote, kote ulimwenguni. Kwa hivyo, nilihisi ni lazima nifanye kitu ambacho kitawakilisha hishima ya UM na wale watumishi wake wanaojitolea mhanga, bila uchoyo, kuimarisha amani ulimwenguni, umma ambao maisha yao yote yalitumiwa kukuza amani na kuhudumia haki za binadamu ili kuhakikisha umma wa kimataifa unaishi maisha bora."

Msanii huyo pia alielezea matumaini aliyonayo kuhusu hisia za watumishi wa UM pamoja jamii za wafanyakazi waliofariki, na wale walionusurika na ajali ya Baghdad, pale watakaposikia muziki wa klasiki aliouandika kwa hishima yao:

"Nitahishimu hisia zao, kama unavyojua, kwa sababu wao ndio waliokuwepo kwenye vuguvugu la ajali [iliotukia Baghda], na ni haki yao kuhisi wanavyopendelea juu ya muziki wangu, lakini pia natumai watasema “Sawa, hivyo ndivyo hasa hisia zetu zilivyo.” Bila shaka kila mtu atakayesikia muziki wangu atahisi tofauti, lakini hilo si tatizo, yote ni sawa. Madhumuni ya mimi kutunga wimbo huu ni kuupatia UM hidaya, kwa kazi nzuri inayofanya kote ulimwenguni, miaka nenda miaka rudi, na ni tunzo maalumu kwa taasisi ya UM na watumishi wake, kijumla."

Sikiliza kibwagizo cha utunzi wa Steve Heitzeg wa muziki wa klasiki uitwao ‘Wimbo usio Mipaka’ kwenye idhaa ya mtandao.