Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

KM BanKi-moon amepongeza taarifa ya Serikali ya Zimbabwe kuondosha vikwazo dhidi ya operesheni za ndani ya nchi za mashirika yasio ya kiserkali na yale mashirika ya binafsi ya kujitolea. Alisema KM maendeleo haya ya kutia moyo yatasaidia kuhakikisha misaada ya kiutu ya kimataifa itagawiwa umma wa Zimbabwe bila upendeleo ili kunusuru maisha na kuwapatia kinga boraya afya.~

Alan Doss, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) amelaumu mapigano yaliozuka karibuni baina ya jeshi la Kongo na wafuasi wa kundi la Chama cha Taifa kwa Ulinzi wa Umma. Doss aliyanasihi makundi yote mawili kujizuia kupigana na kurejea, haraka, kwenye zile sehemu walizokuwepo hapo kabla na kuwataka wajiepushe na vitendo vyote vinavyoweza kushadidia uhasama kwenye eneo hilo.

Radovan Karadzic, aliyekuwa kiongozi wa Serbia, alipofikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa juu ya Iliokuwa Yugoslavia (ICTY) alikataa kujibu kama anakiri makosa au la. Karadzic ametuhumiwa makosa ya vita 11 pamoja na kushiriki kwenye jinai dhidi ya utu, makosa ambayo yanadaiwa kuifanyika kwenye vya Bosnia katika miaka ya 1992-1995.