Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya UM inasema hali katika OPT inazidi kuharibika

Tume ya UM inasema hali katika OPT inazidi kuharibika

Tume ya Wataalamu Watatu wa Kamati Maalumu ya Kuchunguza Vitendo vya Israel dhidi ya Haki za Binadamu za Wafalastina na Waarabu Wengine kwenye Maeneo Yaliokaliwa Kimabavu (OPT) baada ya kukamilisha ziara yao Jordan, na baada ya kusikiliza ushahidi kutoka watu wanaoshidi kwenye maeneo hayo, walibainisha kuwa na wasiwas mkubwa juu ya kuzidi kuharibika kwa hali za kiutu na ukiukaji wa haki za kibinadamu kwenye maeneo husika, hususan katika Tarafa ya Ghaza.

Tangu Kamati Maalumu ya UM ilivyobuniwa hadi hivi sasa, ripoti ilisema, Serikali ya Israel imekataa kushirikiana na Kamati kwenye shughuli zake, na pia kuwanyima wajumbe wa Tume ruhusa ya kuzuru yale maeneo yaliokaliwa kimabavu ya Wafalastina.