Mamilioni Pembe ya Afrika wanahitajia kidharura misaada ya chakula
Jumuiya tisa zinazojumuisha mashirika ya UM yanayoshughulikia misaada ya kiutu, pamoja na mashirika yasio ya kiserekali, Ijumatano yametangaza bia, taarifa ya pamoja inayohadharisha kwamba watu milioni 14 katika mataifa yaliopo Pembe ya Afrika, watahitajia kidharura misaada ya chakula ili kunusuru maisha.