WHO inabashiria Afrika itapungukiwa madaktari hadi 2015
Ripoti ya 2008 ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imeashiria kwamba kuanzia kipindi cha sasa hadi 2015, ambapo Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) yanatarajiwa kukamilishwa, jumla ya madaktari wanaohitajika ulimwenguni kuongoza huduma za afya itakuwa na wizani sawa na idadi ya madaktari watakaopatikana katika kipindi hicho.