Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Adhabu za kifo Marekani zinatathminiwa na Mkariri Maalumu wa Haki za Binadamu

Adhabu za kifo Marekani zinatathminiwa na Mkariri Maalumu wa Haki za Binadamu

Profesa Philip Alston ni Mkariri Maalumu wa UM anayehusika na haki za binadamu zinazofungamana na masuala ya hukumu ya vifo, nje ya sheria, pamoja na mauaji ya kihorera. Majuzi Alston aliwakilisha mbele ya waandishi habari wa kimataifa waliopo Makao Makuu ripoti maalumu iliosailia namna hukumu ya vifo inavyotekelezwa katika taifa la Marekani.

Alibainisha kwamba alizuru majimbo kadha ya Marekani kwa uchunguzi, na alipata fuursa kwenye ziara yake ya kukutana na wenye madaraka wanaoshughulikia mifumo ya sheria. Alithibitisha kuwepo Marekani sheria imara za kutumiwa kuhukumu jinai ya namna kwa namna, kanuni ambazo zimesajiliwa kwenye madaftari ya kihistoria. Lakini pia aligundua kwenye utafiti wake kwamba inapokuja kwenye mas'ala ya hukumu za vifo vya watuhumiwa kadha wa kadha hukosekana kuwepo uwazi wa kuridhisha, unaobainisha vizuri zaidi namna mahakama inavyofikia hukumu hiyo, na ameona wakati mwengine mawakili wanaotetea watuhumiwa vifo hunyimwa fursa halali ya kupokea na kuzingatia taarifa muhimu za ushahidi.

Sikiliza uchambuzi ziada wa Profesa Alston kwenye idhaa ya mtandao.