Skip to main content

Misaada ya kihali kuhudumiwa tena Abyei na UM

Misaada ya kihali kuhudumiwa tena Abyei na UM

Hali ya utulivu imerejea katika eneo la Abyei, Sudan sasa hivi baada ya fujo zilizochipuka huko mwezi Mei. Shirika la Afya Duniani (WHO) likijumuika na mashirika mengine ya UM yameanza kuandaa miradi ya kihali kadha wa kadha ya kuwarudisha makwao maelfu ya watu waliohajiri makazi kufuatia mifumko ya vita siku za nyuma. Mashirika haya yanatarajiwa kuwapatia umma husika huduma za kihali ili kuanzisha maisha kwenye mazingira ya utulivu.