Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UN-HABITAT anaelezea umuhimu wa kudumisha makazi kuimarisha maendeleo

Mkuu wa UN-HABITAT anaelezea umuhimu wa kudumisha makazi kuimarisha maendeleo

Mnamo mwanzo wa wiki Baraza la UM juu ya Maendeleo ya Uchumi na Jamii, yaani Baraza la ECOSOC, lilianzisha mijadala maalumu ya hadhi ya mawaziri, kufanya mapitio ya ripoti za Mataifa Wanachama juu ya mafanikio yaliojiri katika utekelezaji wa kitaifa, na kikanda, kwenye ile ajenda ya UM kuhusu shughuli za maendeleo. Wajumbe wa Baraza hilo walisailia kipamoja hatua za kuchukuliwa kimataifa kuondosha vizingiti vinavyokwamisha ustawi wa uchumi na jamii katika mataifa yanayoendelea.~

Miongoni mwa maofisa wa ngazi za juu wa UM waliohudhuria kikao hiki alikuwemo pia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Makazi (UN-HABITAT) na ambaye vile vile ni Mkuu wa Ofisi za UM za Nairobi, Anna Tibaijuka. Nilipata fursa ya kuwa na mahojiano naye kwenye studio za Redio ya UM hapo Alkhamisi. Kwenye mazungumzo yetu Tibaijuka alitupatia fafanuzi zake kuhusu fungamano ziliopo kati ya kupanda kwa bei za mafuta na chakula duniani, na matatizo ya makazi bora, hususan katika mataifa yanayoendelea.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.