Shambulio la kujitolea mhanga Kabul lashtumiwa na Mkuu wa UNAMA
Kai Eide, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Afghanistan na Mkuu wa Shirika la UM la Kuongoza Misaada katika Afghanistan (UNAMA) ametoa taarifa yenye kushtumu vikali shambulio karaha la bomu la kujitolea mhanga, liliofanyika Kabul Ijumatatu, mbele ya ubalozi wa India, ambapo inaripotiwa watu 40 waliuawa na zaidi ya watu 100 kujeruhiwa. Alisema kitendo hiki kilikuwa ni cha "woga, katili na cha kuchukiza" na ni kitendo ambacho, pia alisema, hakilingani na maadili ya "kiutu, kidini wala kitamaduni."