Mkuu wa ofisi ya UNDP Mogadishu auawa

7 Julai 2008

Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) limelaani vikali mauaji ya Osman Ali Ahmed, yaliotukia Ijumapili kwenye mji wa Mogadishu, Usomali. Ahmed alipigwa risasi kwenye masafa ya uso kwa uso, wakati alipotoka msikitini baada ya sala ya usiku, yeye na mwanawe wakifuatana na mmoja wa wa aila yake,ambao walijeruhiwa kutokana na shambulio hilo.

Marehemu Ahmed alikuwa mkuu wa ofisi ya UNDP Mogadishu, na alijitolea maisha kwa muda mrefu, kutumikia wazalendo wenziwake Usomali ili wapate maisha bora. Mauaji ya Ahmed yanafuata msururu wa mashambulio dhidi ya wafanyakazi wa UM nchini Usomali. UNDP imeitumia aila ya marehemu "mkono wa dhati wa taazia, na kuwaombea nafuu ya haraka mwanawe na nduguye" ambao hivi sasa wanafanyiwa matibabu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter