Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika matatu ya UM yaihimiza G8 kukithirisha vitega uchumi kwenye kilimo

Mashirika matatu ya UM yaihimiza G8 kukithirisha vitega uchumi kwenye kilimo

Wakuu wa mashirika matatu ya UM yanayoshughulikia huduma za kupunguza njaa duniani, yaani mashirika ya IFAD, FAO na WFP, wametoa mwito maalumu kwa viongozi wa mataifa wanachama wa Kundi la G8 wanaokutana hivi sasa kwenye Kisiwa cha Hokkaido, Ujapani unaopendekeza uwekezaji ukuzwe kwenye kilimo, ili kufyeka tatizo la njaa duniani.