Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM amelaani vikali shambulio maututi la walinzi amani Darfur Kaskazini

KM amelaani vikali shambulio maututi la walinzi amani Darfur Kaskazini

Msemaji wa KM, Michele Montas, amearipoti kwenye kikao na waandishi habari wa kimataifa Makao Makuu ya kwamba Ijumanne, Julai 08 (2008) mnamo saa 8:45 alasiri, kwa majira ya Sudan, wanajeshi wa Vikosi Mseto vya UM/UA kwa Darfur (UNAMID) waliokuwa wakifanya doria ya polisi na operesheni za kijeshi, walishambuliwa kwa kuvizia na wanamgambo wasiojulikana katika eneo liliopo kilomita 100 mashariki ya Shangil Tobayi, Darfur Kaskazini, baina ya Gusa Jamat na Wadah.