Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO itafadhilia dola milioni 21 wakulima wadogo wadogo

FAO itafadhilia dola milioni 21 wakulima wadogo wadogo

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limeripoti kupitisha mradi wa dola milioni 21 utakaotumiwa kufadhilia wakulima wadogo wadogo katika nchi 48 huduma za kilimo bora. Miongoni mwa mataifa ya Afrika yatakayopokea msaada huo ni pamoja na Angola, Burundi, Bukini, Comoros, Jamhuri ya Afrika ya Kati na pia Kenya na Zambia.