Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dereva wa WFP wa nne kauawa Usomali

Dereva wa WFP wa nne kauawa Usomali

Majambazi wasiojulikana Ijumatatu walimpiga risasi na kumwua dereva mmoja aliyeajiriwa na Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) katika eneo la Usomali kusini. Dereva huyo anayeitwa Ahmed Saalim alikuwa miongoni mwa madereva waliokuwa kwenye msafara wa WFP, uliochukua tani za metriki 602 za chakula, kutokea Mogadishu na kuelekea kwenye maeneo ya Bakooll na Bay na kuwapatia umma muhitaji lishe ya kunusuru maisha.