Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kupongeza msimamo wa G8 kuhusu mzozo wa chakula duniani

WFP kupongeza msimamo wa G8 kuhusu mzozo wa chakula duniani

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limepongeza ahadi zilizotolewa na viongozi wa kimataifa kwenye mkutano wa G8 uliofanyika Ujapani wiki hii, ambapo waliafikiana kuunga mkono juhudi za kupunguza makali ya athari za bei kubwa za chakula katika nchi masikini, na kukubali kuyapatia mataifa hayo suluhu ya muda mrefu.