Kikao cha CEDAW chazingatia haki za wanawake Tanzania

11 Julai 2008

Wawakilishi kadha wa kimataifa walikusanyika kwenye Makao Makuu ya UM kuanzia tarehe 30 Juni kuhudhuria kikao cha mwaka cha Kamati ya Kuondosha Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW), kwa madhumuni ya kufanya mapitio juu ya namna Mataifa Wanachama yalioridhia Mkataba wa CEDAW yanavyowatekelezea wanawake haki zao. Miongoni mwa Mataifa manane yaliowakilisha ripoti za mapitio mbele ya Kamati mwaka huu, kwenye kikao cha 41, ilijumuisha pia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vikao vya Kamati ya CEDAW vile vile vilihudhuriwa na wajumbe waliowakilisha mashirika yasio ya kiserekali kutoka Tanzania. Nilibahatika kuwa na mahojiano kwenye studio zetu na wajumbe wawili wa mashirika hayo ambao walitupatia fafanuzi halisi kuhusu ufahamivu wao wa namna haki za wanawake zinavyotekelezwa Tanzania.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter