14 Julai 2008
Msemaji wa KM ametoa ripoti yenye kukanya shtumu za Mjumbe wa Kudumu wa Zimbabwe katika UM, Balozi Boniface G. Chidyausiku ambaye alishuku namna KM Ban Ki-moon alivyojihusisha, kwa tuhuma za upendeleo, kuunga mkono baadhi ya wahusika wa matukio yaliojiri karibuni Zimbabwe, madai ambayo Msemaji wa KM alisisitiza “hayakubaliki na yasiofaa”.