Skip to main content

Tathmini za Mkuu wa UN-HABITAT juu ya UNCTAD XII

Tathmini za Mkuu wa UN-HABITAT juu ya UNCTAD XII

Mkutano wa 12 wa Shirika la UM juu ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD XII)ulifanyika mwaka huu mwezi Aprili katika mji wa Accra, Ghana. Asilimia kubwa ya wajumbe kutoka Mataifa Wanachama walikusanyika kuzingatia kipamoja matatizo yanayoambatana na ukosefu wa usawa kwenye soko la kimataifa, na athari zake kwenye huduma za maendeleo, hasa katika nchi masikini.

Ripoti ya UM ya Utafiti wa 2008 juu ya Maendeleo ya Uchumi na Jamii Duniani ilipendekeza kupatikane marekibisho kwenye sera za kimataifa, kijumla, ili kuhakikisha kurejea utulivu mkuu wa uchumi na usalama duniani, kutoka mazingira ya sasa yaliovuna vitisho hatari kwa nchi masikini, vinavyochochewa zaidi na kupanda kwa kasi kwa bei za chakula na nishati, pamoja na watu kushindwa kulipa mikopo kinga ya nyumba katika nchi zenye maendeleo ya viwanda, na kufilisika kwa mabenki. KM Ban Ki-moon kwenye risala yake mbele ya kikao cha UNCTAD XII alipendekeza Afrika izingatie hatua za haraka kufufua uchumi na maendeleo barani humo. KM alipendekeza uwekezaji na shughuli za biashara, hasa katika sekta ya kilimo, uongezwe, kadhia ambayo anaamini ikitekelezwa kikamilifu itayavua mataifa ya Afrika, hususan yale yalio dhaifu kiuchumi katika kusini ya Sahara, na mzigo wa umaskini na hali duni.

Anna Tibaijuka, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Makazxi (UN-HABITAT) naye vile vile alihudhuria Mkutano wa UNCTAD XII mjini Accra. Mwandishi Habari wa Redio ya UM, Don Bobb, alipata fursa ya kufanya mahojiano na Tibaijuka, ambaye alitupatatia fafnuzi zake halisi kuhusu kikao na matumaini aliyonayo katika siku za mbele kuhusu maendeleo patakapopatikana marekibisho yanayofaa, hasa katika udhibiti bora wa biashara kwenye soko la kimataifa.

Sikiliza jawabu kamili za Tibaijuka kwenye idhaa ya mtandao.