UNICEF/WHO yatoa ripoti kuhusu usafi na maji duniani

17 Julai 2008

Alkhamisi Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), likichanganyika na WHO, yamewasilisha ripoti bia mpya inayoelezea maendeleo yaliopatikana katika juhudi za kuhudumia umma wa kimataifa maji safi na usafi wa mastakimu, huduma ambazo ni muhimu kwa afya ya watu binafsi pamoja na jamii.

Ama kuhusu maendeleo katika huduma za maji safi na salama ripoti ya UNICEF/WHO juu ya usafi na maji salama imetambua na kupongeza nchi saba, kati ya mataifa kumi yaliopo kusini ya Sahara, kwa kufanikiwa kupiga hatua kubwa kwenye juhudi za kutekeleza, kwa wakati, lengo la kuupatia umma wao maji safi na salama. Mataifa hayo hujumuisha Burkina Faso, Namibia, Ghana, Malawi, Uganda pamoja na Mali na Djibouti, nchi ambazo, ripoti ilisema, zipo kwenye mkondo sawa unaotakikana kukamilisha lengo la MDGs kuupatia umma maji safi na salama katika 2015, licha ya kuwa nchi hizi zimezongwa na vizingiti aina kwa aina kwenye mazingira magumu kiuchumi na kijamii.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter