Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera ya EU kudhibiti wahamiaji yashtusha wataalamu wa haki za binadamu wa UM

Sera ya EU kudhibiti wahamiaji yashtusha wataalamu wa haki za binadamu wa UM

Wataalamu kumi wanaohusika na Masuala Makhsusi ya Baraza la Haki za Binadamu wamemtumia barua maalumu Raisi wa Baraza la Umoja wa Ulaya, uraisi ambao unashikwa na Ufaransa kwa sasa, inayobainisha wasiwasi wao kuhusu pendekezo la \'Mwongozo wa EU juu ya Udhibiti wa Uhamiaji\' kwenye nchi wanachama wa EU. Sera imependekeza mataifa yote yakubali kutekeleza kipamoja sheria za kuwarejesha makwao, bila khiyari, wale raia wwenye kuishi kwenye mataifa ya EU ambao waliokiuka ruhusa ya muda wa ukaazi.

Antonio Guterres, Kamishna Mkuu wa UNHCR alikutana wiki hii na Raisi wa Baraza la Ulaya, Jose Manuel Barroso ambaye alimshukuru kwa taasisi yao kuendelea kufadhilia msaada wa kuhudumia wahamiaji. Kwa wakati huo huo Guterres allilitaka EU pia ihakikishe raia wa kigeni wenye kuomba hifadhi ya kimataifa hawatonyimwa haki hiyo.