Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msanii wa Sudan Kusini ataka biashara ya silaha ndogo ndogo ikomeshwe

Msanii wa Sudan Kusini ataka biashara ya silaha ndogo ndogo ikomeshwe

Wiki hii kwenye Makao Makuu ya UM kulifanyika mkutano wa kutathminia hatua za kukomesha matatizo yanayoambatana na biashara haramu ya silaha ndogo ndogo. Mkutano huu hujumuisha Mataifa Wanachama kila miaka miwili ambapo huwapatia wajumbe wanaohudhuria kikao fursa ya kubadilishana mawazo juu ya uzoefu walionao, na kujadilia namna ya kukwamua vile vizingiti vyenye kutatanisha utekelezaji wa Mpango wa Utendaji wa 2001 (PoA) dhidi ya biashara haramu ya silaha ndogo ndogo duniani, silaha ambazo pia hutumiwa kupalilia vita na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika nchi masikini.~

Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria kikao cha mwaka huu alikuwemo msanii wa muziki wa hip hop, kutokea Sudan Kusini, Emmanuel Jal. Tulipata fursa ya kumhoji kwenye studio zetu. Emmanuel ni miongoni mwa wale vijana ambao walipokuwa wadogo walilazimishwa kushiriki kwenye mazingira ya kiwewe na kihoro ya vita nchini mwao.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.