Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA itapeleka wataalamu Syria kuchunguza madai ya shughuli za siri

IAEA itapeleka wataalamu Syria kuchunguza madai ya shughuli za siri

Mohamed ElBaradei, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) Ijumatatu aliwasilisha ripoti yake mbele ya wajumbe 35 wa Bodi la Utendaji, linalokutana hivi sasa mjini Vienna kuhusu kazi za taasisi. Aliarifu kwamba mwezi Aprili IAEA ilipokea taarifa zilizodai "kituo cha umeme” nchini Syria, kilchoipigwa makombora na ndege za Israel mwezi Septemba 2007, kilikuwa kikiendeleza shughuli zisio halali. Kwa sababu hizo, alisema ElBaradei, kuanzia Juni 22 hadi 24, IAEA itapeleka tume maalumu ya wataalamu kuchunguza kama kuna uwkeli kutokana na tetesi za Marekani na Israel zilizodai Syria ilishiriki kwenye huduma za siri za kinyuklia.