Ripoti mpya kumurika mafanikio/pingamizi katika kupiga vita UKIMWI

2 Juni 2008

Ripoti iliotayarishwa bia na Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya UKIMWI (UN-AIDS), pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) imethibitisha mnamo mwisho wa 2007, watu milioni 3 wenye virusi vya UKIMWI, katika nchi zinazoendelea za pato la chini na kati kiuchumi, walifanikiwa kupatiwa zile dawa maalumu za kurefusha maisha, dawa zijulikanao kwa umaarufu kama dawa za ARV.

Kadhalika ripoti ilisema mafanikio yamepatikana kwenye huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka mama-kwa-mtoto. Huduma za kupima maradhi ya UKIMWI zimepanuliwa, iliongeza kusema ripoti, na watu walioambukizwa virusi wanaopatiwa ushauri imekithiri, halkadhalika. Vile vile ripoti imebainisha kuimarishwa zile juhudi za kuhakikisha watot wa kiume wanatahiriwa kwenye maeneo ya Afrika kusini ya Sahara yalioathirika zaidi na maambukizi ya UKIMWI.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter