Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya udhibiti wa athari za hali ya hewa duniani yaanzishwa Bonn

Mazungumzo ya udhibiti wa athari za hali ya hewa duniani yaanzishwa Bonn

Leo mjini Bonn, Ujerumani kumefunguliwa mkutano wa wiki mbili wa UM kuzingatia hatua za kuchukuliwa kipamoja, kuandaa taratibu za kudhibiti bora tatizo la uharibifu unaoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Kadhalika katika wiki mbili zijazo mazungumzo yataendelea miongoni mwa Mataifa Yalioidhinisha Mkataba wa Kyoto juu ya masharti ya utekelezaji wa mapendekezo ya Makataba. Mkutano wa Bonn umeandaliwa na Taasisi ya UM ya juu ya Mkataba wa Kudhibiti Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani (UNFCCC).