Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama linazingatia masuala ya amani kwa Usomali

Baraza la Usalama linazingatia masuala ya amani kwa Usomali

Ijumatatu, ujumbe wa Baraza la Usalama unaozuru Afrika, ulikutana kwa mashauriano na viongozi wa Usomali ambao walikusanyika Djibouti kuhudhuria mazungumzo yanayosimamiwa na UM kuhusu usalama na amani ya Usomali. Ujumbe wa Baraza la Usalama ulikutana na wawakilishi wa Serikali ya Mpito pamoja na wajumbe wa upinzani.

Kadhalika, Baraza la Usalama limepitisha azimio linalolaani vitendo vya uharamia na wizi wa mabavu vinavyofanyika kwenye mwambao wa Usomali, jinai ambayo, azimio lilisema, inakwamisha zile huduma za mashirika ya kimataifa za kupeleka misaada ya kiutu kwa umma muhitaji. Azimio limependekeza pia kwa mataifa yanayoshirikiana na Serikali ya Mpito ya Usomali kuchukua kila hatua inayofaa kisheria, kupambana na uharamia unaotukia kwenye maeneo ya mwambao yalio chini ya utawala wa Usomali.