Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ahimiza Mkutano wa Roma kuongeza kilimo kuepusha njaa

KM ahimiza Mkutano wa Roma kuongeza kilimo kuepusha njaa

Kwenye hotuba ya ufunguzi Ijumanne mjini Roma, Utaliana kwenye Mkutano Mkuu juu ya Udhibiti Bora wa Akiba ya Chakula Duniani KM Ban Ki-moon aliyahimiza Mataifa Wanachama kuekekza zaidi kwenye kilimo kitachosaidia kuzalisha chakula zaidi kwa kipindi cha muda mrefu ujao, ili kuepukana na janga la njaa ambalo, katika siku za karibuni, limeoshuhudiwa likipalilia machafuko na vurugu katika sehemu mbalimbali za dunia:~