Ukiukaji wa haki za binadamu pia huchochea njaa, kuonya Kamishna Mkuu

4 Juni 2008

Louise Arbour, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu alisema kwamba mara nyingi ukiukaji wa haki za binadamu unaoendelezwa na baadhi ya serikali wanachama, huwa ndio vyanzo vya migogoro ya chakula ndani ya mataifa hali ambayo, baadaye, huzorotisha zile juhudi muhimu za kukidhi mahitaji ya chakula kwa umma. Risala ya Arbour iliwasilishwa mbele ya viongozi wa kimataifa pamoja na wawakilishi wa vyeo vya juu waliokusanyika Roma kwenye mkutano wa kusailia mzozo wa chakula duniani.~ ~

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter